Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 29, 2025 Local time: 19:40

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa asema wanashirikiana  taarifa za kijasusi na Ukraine

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov na Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu wakihutubia mkutano na waandishi wa habari kama sehemu ya ziara rasmi ya Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Hoteli de Brienne mjini Paris Januari 31, 2023.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu alisema Alhamisi kwamba Ufaransa inashirikiana  taarifa za kijasusi na Ukraine, hatua iliyofuatia baada ya Marekani kusema inapunguza ushirikiano wa  kijasusi na Ukraine.

Hatua hiyo inakuja wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya walipokusanyika Alhamisi mjini Brussels, pamoja na

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwenye mkutano ili kujadili kuimarisha ulinzi matumizi na kuimarisha ahadi za kuiunga mkono Ukraine katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Russia.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kabla ya mazungumzo hayo kuwa wanachama wa EU watachukua hatua madhubuti kusonga mbele huku akielezea wasiwasi wake juu ya mabadiliko ya msaada wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG