China itaongeza juhudi zaidi kwa ajili ya kuungana kwa amani na Taiwan lakini itachukua hatua zote muhimu kulinda uadilifu wa eneo la China, wizara yake ya mambo ya nje ilisema Jumatatu. China inadai Taiwan kama eneo lake licha ya pingamizi kutoka serikali ya Taipei.
Rais wa Taiwan Lai Ching-te amesema ni watu wa Taiwan pekee wanaoweza kuamua mustakabali wao. Wiki iliyopita pembeni mwa mkutano wa kila mwaka wa bunge la China, Waziri wa Mambo ya Nje, Wang Yi aliwaambia waandishi wa habari kwamba Taiwan haitakuwa nchi, na uungaji mkono uhuru wa Taiwan ilikuwa kuingilia mambo ya ndani ya China.
China iko tayari kufanya kila tuwezalo kujitahidi kwa matarajio ya kuungana tena kwa amani na uaminifu mkubwa, alisema Mao Ning, msemaji wa wizara ya mambo ya nje alipoulizwa kuhusu matamshi ya Wang juu ya Taiwan.
Forum