Maafisa wa Russia na Ukraine wameripoti mapigano katika mkoa wa Sumy nchini Ukraine huku kusonga mbele kwa Russia katika eneo hilo kumesababisha uwezekano wa kukata laini za usambazaji huduma kwenda jeshi la Ukraine.
Maafisa wanasema mapigano yalikuwa yakiendelea katika eneo la Novenke. Sumy iko katika mpaka kutoka mkoa wa Kursk nchini Russia mahala ambako vikosi vya Ukraine vilianzisha mashambulizi mwezi Agosti. Vikosi vya Russia vilitwaa sehemu za Sumy katika kipindi cha mwanzo cha uvamizi wao kamili kwa Ukraine ambao ulianza zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Jeshi la Ukraine limesema Jumatatu kuwa lilitungua ndege 130 za Russia zisizokuwa na rubani usiku wa kuamkia leo ambazo zililenga maeneo mbalimbali nchini humo. Muingiliano ulifanyika katika mikoa ya Cherkasy, Chernihiv, Dnipropetrovsk, Kharkiv, Kherson, Kirovohrad, Kyiv, Mykolaiv, Odesa, Poltava, Sumy, Vinnytsia na Zaporizhzhia, jeshi lilisema.
Forum