Papa Francis anashiriki katika wiki ya mapumziko ya kiroho huko Vatican kutoka hospitali ya Roma wakati akiendelea kupona Jumatatu kutokana na homa ya mapafu mara mbili na anatazamia maadhimisho ya miaka 12 ya uchaguzi wake huku kukiwa na maswali kuhusu hali ya baadae ya upapa wake.
Papa Francis alifuatilia ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya video siku ya Jumapili. Alimuona na kumsikiliza Mchungaji Roberto Pasolini, mhubiri wa kaya ya kipapa, lakini mapadri, maaskofu na makadinali katika ukumbi wa Vatican hawakuweza kumwona wala kumsikia.
Pasolini alitoa tafakari juu ya Matumaini ya uzima wa milele, mada ambayo ilichaguliwa kabla ya Francis kulazwa katika hospitali ya Gemelli huko Roma hapo Februari 14 kutokana na maambukizi katika mapafu.
Mapumziko hayo ambayo ni mkusanyiko wa kila mwaka unaoanza msimu wa kwaresma katika Kanisa Katoliki kuelekea Pasaka unaendelea kwa wiki kadhaa. Vatican imesema kuwa Francis atashiriki katika ushirika wa kiroho Pamoja na uongozi wote wakiwa mbali.
Forum