Mwanasheria mkuu wa Sudan, Tagelsir al-Hebr, amewaambia waandishi wa Habari jana kuwa washukiwa walikuwa na vilipuzi vya kutosha kuuharibu mji mkuu, Khartoum.
Msemaji wa kikosi cha jeshi Rapid Support Forces, amesema uchunguzi wa Agosti juu ya harakati za makundi va kigaidi ulipelekea ukamataji huo.
Jamal Jumaa, amesema kuna wasi wasi baadhi ya raia wa Sudan, wataanza kulipua mabomu baada ya washukiwa kupatikana na shehena kubwa ya vilipuzi ambavyo vingeweza kusababisha uharibifu.
Wanalinganisha shehena za vilipuzi hivi sawa na mlipuko wa Lebanon uliotokea mwezi uliopita katika bandari ya Beirut, ambao uliua watu wasiopungua 190 na kuacha sehemu kubwa ya jiji ikiwa kifusi kutokana na mlipuko wa amonia nitrate.