DRC yatangaza zawadi kwa kufanikisha kukamatwa viongozi wa waasi

AFC Leader Corneille Nangaa announcing new local leaders in the rebel held area - 02-06-2025. Photo: Jimmy Shukran Bakomera

Serekali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatoa zawadi ya dola milioni tano kwa atakaye saidia kuwakamata viongozi wa kundi la M23 ambalo limeteka miji miwili mikubwa ya majimbo ya Kivu, Wizara ya sheria imetangaza.

“Zawadi ya dola milioni tano itatolewa kwa mtu yeyote anayesaidia kuwakamata wahalifu Corneille Nangaa, Bertrand Bisimwa na Sultani Makenga,” imesema taarifa ya wizara hiyo iliyoandikwa Ijumaa.

Nangaa, kiongozi katika Muungano wa River Congo (AFC) ambao ni muungano wa kijeshi na kisiasa ambao M23 wanashiriki, ni rais wa zamani wa tume ya uchaguzi ya DRC. Bisimwa na Makenga mtawalia ni rais na mkuu wa kijeshi wa kundi la M23.

Walipohukumiwa bila kuwepo Kinshasa, wote watatu walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifo Agosti 2024.

Serekali ya DRC pia inatoa zawadi ya dola milioni nne kwa taarifa zozote zitakazowezesha kukamatwa kwa wasaidizi wa watu hao watatu na watu wengine wanaotafutwa, imesema taarifa hiyo.