Mapigano yalizuka Jumanne mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku tatu baada ya wito wa viongozi wa Afrika wa kusitisha mapigano na utulivu kwa muda mfupi katika mzozo huo.
Hali ilionekana kuwa tulivu Jumatatu kwa siku ya pili huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya viongozi wa SADC na Jumuia ya Afrika Mashariki kutoa wito wa sitisho la mapigamo kutokana na hofu kuwa mapigano yanaweza kuchochea mzozo mkubwa.
Hamas Jumatatu ilisema itachelewesha mpango wa kuwaachilia mateka zaidi katika Ukanda wa Gaza baada ya kuishtumu Israel kwa kukiuka makubaliano ya sitisho la mapigano ambayo kwa sasa yanakabiliwa na mzozo wake mkubwa zaidi tangu yaanze kutelezwa wiki tatu zilizopita.
Sam Nujoma ambaye aliongoza mapambano ya miongo mitatu ya kupigania uhuru wa Namibia kutokea Afrika Kusini yenye ubaguzi wa rangi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, ofisi ya rais ilitangaza Jumapili.
Mapigano makali huko kusini na magharibi mwa Sudan yaliua watu 65 na kujeruhi wengine zaidi ya 130 Jumatatu, madaktari wamesema, huku vita vibaya kati ta jeshi na kundi la wanamgambo vikipamba moto tena.
Rwanda Jumapili imekubaliana na pendekezo la kufanyika kwa mkutano utakaosimamiwa na SADC na Jumuia ya Afrika Mashariki kujadili mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku Tanzania ikitangaza pia kwamba wanajeshi wake wawili waliuawa katika mapigano ya hivi karibuni.
Kundi la waasi wa M23 Alhamisi limeapa kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, huku wapiganaji wake wakisonga mbele zaidi katika eneo la mashariki mwa nchi lenye utajiri wa madini.
Jaji Jumatano amemhukumu seneta wa zamani wa Marekani mwenye ushawishi mkubwa kifungo cha miaka 11 jela, baada ya kukutwa na hatia ya rushwa kufuatia kugunduliwa kwa dhahabu nyingi na maelfu ya dola pesa taslimu nyumbani kwake.
Jumuia ya Afrika Mashariki Jumatano imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzungumza na “wadau wote”, wakiwemo wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, ili kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi.
Kundi la waasi wa M23 limesonga mbele kwenye uwanja mwingine wa mapambano huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa kuteka wilaya mbili katika jimbo la Kivu Kusini, vyanzo vya eneo hilo vimeiambia AFP Jumatano.
Maelfu ya watu katika nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zinazoongozwa na serikali za kijeshi Jumanne waliandamana kuunga mkono uamuzi wa nchi hizo wa kujiondoa kwenye Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Kundi la waasi wa M23 Jumanne lilichukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa mji wa Goma, chanzo cha usalama kimesema, kufuatia mapigano ya siku tatu ambayo yameua zaidi ya watu 100.
Wizara ya sheria ya Marekani Jumatatu iliwafuta kazi maafisa kadhaa waliohusika katika kesi za mashtaka ya jinai dhidi ya Rais Donald Trump.
Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh amesema ana nia ya kuchukua tena udhibiti wa chama chake cha siasa na kutangaza kwamba “anarudi nyumbani”, katika ujumbe wa sauti ambao shirika la habari la AFP limeupata Alhamisi.
Sudan Kusini Jumatano imeamuru kampuni zinazotoa huduma za intaneti kuzuia mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook na TitTok, kufuatia maandamano yenye vurugu yaliyochochewa na vifo vya raia wake wiki iliyopita.
Maelfu ya watu wameuwawa na wengine zaidi ya milioni 12 wamekoseshwa makazi kutokana na mzozo uliozuka baina ya jeshi la Sudan na kundi la waasi tangu April mwaka 2023.
Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimefanya uchaguzi mkuu na kumchagua kiongozi mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa mwezi Oktoba mwaka huu wakati ambapo chama kinakabiliwa na ongezeko la ukandamizaji wa kisiasa.
Nchi tatu zinazotawaliwa na wanajeshi katika kanda ya Sahel zitaungana kuunda kikosi cha wanajeshi 5,000 kupambana na ghasia za wanajihadi ambazo zimekumba mataifa hayo kwa miaka kadhaa, maafisa walisema Jumanne.
Rwanda Jumatano ilibadili kauli kufuatia madai yake ya awali kwamba iligundua akiba yake ya kwanza ya mafuta katika Ziwa Kivu, ikisema bado iko kwenye awamu ya uchunguzi na inatafuta washirika.
Shirika la afya duniani WHO Jumanne limesema kwamba mlipuko unaoshukiwa wa ugonjwa hatari wa Marburg nchini Tanzania umewaua watu wanane, na kuonya kwamba hatari ya kusambaa kwa ugonjwa huo nchini humo ni “kubwa”.
Pandisha zaidi