Maafisa wa Ufilipino wanasema Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekamatwa Rodrigo Duterte aliondoka mjini Manila akiwa ndani ya ndege na atakabidhiwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mjini The Hague.
Israel Jumapili ilitangaza kwamba imekata huduma ya umeme kwa Gaza. Matokeo ya hatua hiyo hayakueleweka haraka, lakini eneo la Gaza linapata umeme kutoka Israel ili kuzalisha maji ya kunywa.
Waumini wa kanisa katoliki wamekuwa na hisia mchanganyiko baada ya kusikia sauti ya Papa Francis leo Ijumaa, kwa mara ya kwanza tangu alipolazwa hospitali, mwezi Februari.
Rais wa serikali ya mpito ya Syria Ahmad al-Sharaa amewasili Cairo kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Kiarabu.
Watu 11 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa Alhamisi wakati wa mlipuko katika mji wa mashariki mwa Congo wa Bukavu uliotokea kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na viongozi wa kundi la M23, ambalo lilichukua udhibiti wa mji huo mapema mwezi huu.
Serikali ya Uganda imesema Jumatano kwamba mmoja wa wake na watoto watatu wa kiongozi wa uasi kutoka Uganda Joseph Kony wamerejeshwa Uganda kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Maseneta wa chama cha Republican wamepitisha bajeti ya dola bilioni 340 ambazo utawala wa Rais Donald Trump umesema unahitaji kwa ajili ya kufanikisha mpango wake wa kuwarudisha makwao wahamiaji haramu walio Marekani, na kwa ajili ya usalama mpakani.
Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Marco Rubio hatohudhuria Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa G20 utakaofanyika Afrika kusini wiki hii huku kukiwa na mivutano inayoendelea baina ya mataifa hayo mawili.
Hamas Alhamisi ilisema itawaachilia mateka watatu zaidi wa Israel mwishoni mwa juma kama ilivyopangwa kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina.
Umoja wa Mataifa Jumatatu ulisema umesitisha shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo ambalo ni ngome ya waasi wa Kihouthi wa Yemen baada ya waasi hao kuwashikilia wafanyakazi wanane wa Umoja huo.
Kiongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi UNAIDS Jumatatu amesema kwamba kesi mpya za maambuikizi ya HIV na Ukimwi huenda zikaongezeka kwa zaidi ya mara 6 kufikia 2029.
Mamlaka nchini Libya zilipata karibu miili 50 kwenye makaburi mawili ya watu wengi katika jangwa la kusini mashariki mwa nchi hiyo, maafisa walisema Jumapili.
Marekani imeufahamisha rasmi Umoja wa Mataifa kwamba imesitisha ufadhili wake kwa kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambacho kilikuwa na jukumu la kupambana na magenge yanayojaribu kudhibiti mji mkuu wa Haiti, Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne.
Mamia ya majeruhi Jumatatu walionekana wakimiminika katika hospitali zilizojaa watu huko Goma, mji mkuu wa mashariki mwa Kongo, huku mapigano yakiendelea kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao waliuteka mji huo wenye takriban watu milioni 2.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili alisema kwamba ameamuru ushuru, marufuku ya viza na hatua nyingine za ulipizaji kisasi zichukuliwe dhidi ya Colombia baada ya serikali ya nchi hiyo kuzikatilia ndege mbili zilizokuwa zinabeba wahamiaji kuingia nchini humo.
Rais mteule Donald Trump Jumanne ametangaza mipango ya kuunda idara mpya inayoitwa “ Idara ya mapato ya nje” kukusanya ushuru na mapato mengine kutoka mataifa ya kigeni.
Watu 100 ambao walikuwa wakichimba madini kinyume cha sheria katika mgodi wa dhahabu usiofanya kazi nchini Afrika Kusini walifariki baada ya kunaswa chini ya mgodi huo kwa miezi kadhaa, huku polisi wakijaribu kuwaondoa huko, kundi linalowakilisha wachimba migodi hao lilisema Jumatatu.
Chama tawala nchini Chad kimepata viti vingi katika uchaguzi wa bunge wa mwezi Disemba, ambao ulisusiwa na vyama vikuu vya upinzani ambapo wachambuzi wanasema utaimarisha nguvu za kisiasa za rais, matokeo ya awali yameonyesha.
Jaji wa Mahakama ya New York amemhukumu Donald Trump kuachiliwa bila ya masharti yoyote leo Ijumaa kwa kuficha malipo ya pesa kwa mcheza filamu za ngono licha ya juhudi za rais-mteule wa Marekani kufanya juhudi za dakika za mwisho kuepuka kuwa mhalifu wa kwanza katika White House.
Congo Alhamisi imeipiga marufuku mtandao wa habari wa Al Jazeera kutokana na kutanganza mahojiano yake na kiongozi wa kundi la uasi ambalo limekamata eneo la mashariki mwa nchi katika siku za karibuni.
Pandisha zaidi