ratiba ya matangazo
Uganda yaadhimisha miaka 60 ya uhuru wake
Uganda imesheherekea miaka 60 ya Uhuru wake Jumapili huko katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.Rais Yoweri Museveni katika hotuba yake alitoa wito wa ushirikiano wa kibiashara kwa mataifa ya Afrika Mashariki na kuacha utegemezi wa kuagiza bidhaa kutoka nje ya kanda hiyo.
Dunia yaadhimisha siku ya afya ya akili
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya afya ya akili, mataifa ya Afrika yaelezwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojiua huku wengine wakiwa hawafahamu kuwa na tatizo. Mjadala waibuka baada ya kauli ya rais wa Kenya William Ruto kusema Afrika mashariki iwe nchi moja na mipaka kuondolewa.
Dunia inaadhimisha siku ya afya ya akili kwa kauli mbiu isemayo "Fanya afya ya akili na ustawi kwa wote kuwa kipaumbele cha kimataifa".
Wataalamu katika sekta ya afya ya akili na waathirika wa tatizo hili wanazungumzia baadhi ya sababu zinazoibua afya ya akili kwa binadamu, changamoto zilizopo kwa jamii na nini kifanyike kusitisha tatizo la afya ya akili kwa umma