ratiba ya matangazo
16:30 - 16:59
Rais wa Marekani Joe Biden anahudhuria mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa mataifa (COP27) nchini Misri
Rais Biden anazungumzia kuhusu kile Marekani imefanya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ndani ya Marekani na nje ya nchi. Baadhi ya wajumbe wa mkutano wapo na ari ya kusikia kile mataifa tajiri yanaweza kufanya kwa mataifa ambayo yanakabiliwa na maafa ya mazingira.
19:30 - 20:29
Mjadala kuhusu uchaguzi wa katikati ya mhula hapa Marekani, wakati ushindani ukiendelea kukaribiana kati ya Demokrat na Repablikan
Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.