Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir Jumatano limesema kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefunga anga yake kwa ndege zake zote, huku mzozo mashariki mwa DRC ukiongezeka.
Katika hatua mpya ya kutafuta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamefikia maamuzi yatakayosaidia kurejesha utulivu katika eneo hilo linalokumbwa namzozo wa muda mrefu.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, na mwenzake wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, walishiriki mkutano wa Jumamosi, Tanzania, ambapo viongozi wa kikanda walitoa mwito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini DRC.
Rwanda Jumapili imekubaliana na pendekezo la kufanyika kwa mkutano utakaosimamiwa na SADC na Jumuia ya Afrika Mashariki kujadili mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku Tanzania ikitangaza pia kwamba wanajeshi wake wawili waliuawa katika mapigano ya hivi karibuni.
Kundi la waasi wa M23 Alhamisi limeapa kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, huku wapiganaji wake wakisonga mbele zaidi katika eneo la mashariki mwa nchi lenye utajiri wa madini.
Jumuia ya Afrika Mashariki Jumatano imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuzungumza na “wadau wote”, wakiwemo wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, ili kumaliza mapigano katika eneo la mashariki mwa nchi.
Kundi la waasi wa M23 Jumanne lilichukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa mji wa Goma, chanzo cha usalama kimesema, kufuatia mapigano ya siku tatu ambayo yameua zaidi ya watu 100.
Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC imelaani “kitendo cha uvamizi cha waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.
Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alisema kwamba mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo katika mji mkuu muhimu wa mashariki mwa nchi yalikuwa “hayajamalizika”, licha ya waasi hao kudai kwamba waliuteka mji wa Goma.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumapili limewataka waasi wa M23 kusitisha mashambulizi yao na kuacha kusonga mbele kuelekea mji wa Goma, mji mkubwa wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuomba majeshi ya kigeni kuondoka mara moja.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa siku ya Jumamosi, maafisa wa Congo walilaani kuhusika kwa Rwanda katika mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako mapigano kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 yameongezeka.
Mamia ya watu walikuwa wanajaribu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenda Rwanda siku ya Jumapili, huku mapigano makali yakiendelea kote katika mji muhimu wa Mashariki mwa Congo wa Goma, kilometa chache kutoka mstari wa mbele.
Pandisha zaidi