Akiwa Kenya atazungumza na wanawake na kutembelea maeneo yanayokumbwa na ukame na baadhi ya miradi inayogharimiwa na Marekani. Akizungumza na mwandishi habari wa shirika la habari la AP kwa mara ya kwanza alifafanua bayana kwamba mumewe Biden yuko tayari kugombania mhula wa pili.
Jill Biden mke wa rais wa Marekani awasili Nairobi, Kenya kituo cha pili cha ziara ya Afrika
- Abdushakur Aboud
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden amewasili Nairobi Ijumaa tarehe 24, Februari akiwa katika ziara ya mataifa mawili ya Afrika, Namibia na Kenya akifuatana na mjuku wake Naomi

1
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden awasili Kenya Ijuma Feb 24, kituo cha pili cha ziara yake ya Afrika

2
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akikaribishwa Nairobi Kenya.

3
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akaribishwa na mwenzake wa Kenya Rachel Ruto na wanatumbwizwa na wacheza ngoma za kienyeji kwenye uwanja wa ndege wa Nairobi.

4
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden akisalimiwa na wanafunzi, alipotembelea chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia mjini Windhoek, Namibia.