Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 29, 2025 Local time: 17:57

Changamoto za ulezi wa watoto walemavu kiakili Kenya


Changamoto za ulezi wa watoto walemavu kiakili Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:41 0:00

Wanawake wanaowalea watoto walemavu katika jamii za kipato cha chini wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinatatiza uwezo wao wa kushughulikia watoto hao. Changamoto hizo zinataabisha wanawake kimawazo, na kihisia wanapotengwa na jamii huku matatizo hayo yakiishia kuwadhuru watoto walemavu.

Mwanidshi wa Sauti ya Amerika mjini Mombasa Salma Mohamed ametembelea kituo kimoja cha kuwashughulikia watoto wanaogua utindio wa ubongo yaani cerebral Palsy na kutuandalia ripoti ifuatayo.

Kurunzi ni kituo cha afya ya viungo kwa watoto wanaoishi na utindio wa Ubongo maarufu cerebral palsy katika kitongoji kimoja mjini Mombasa.

Hapa watoto hao wenye ulemavu huo hufanyiwa matibabu ya kunyoosha mwili na viungo kama njia moja ya kuhakikisha miili yao inasalia katika hali nzuri. Ingawa kurunzi ni zahanati ya watoto wa Cerebral Palsy, hii pia ni sehemu maalum kwa wanawake kupata usaidizi wa kihisia na kimawazo.

Forum

XS
SM
MD
LG