Kesi hiyo inatokana na mashtaka mawili yaliyofikishwa mbele ya seneti kuhusiana na kadhia ya Ukraine ambapo inadaiwa Rais Trump alitumia vibaya madaraka yake kwa kuzuia msaada wa kijeshi kwenda Ukraine.
Baraza la Seneti : Matukio muhimu ya kesi inayoendelea dhidi ya Rais Donald Trump
Baraza la Seneti la Bunge la Marekani laanza kusikiliza hoja za awali juu ya kesi inayotaka kumuondoa Rais Donald Trump madarakani, Jumatano, Januari 22, 2020.

1
Baraza la Seneti la Bunge la Marekani laanza kusikiliza hoja za awali juu ya kesi ya inayotaka kumuondoa Rais Donald Trump madarakani, Jumatano, Januari 22, 2020.

2
Karani wa Bunge Cheryl Johnson akishikilia nyaraka za mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump kwa ajili ya kuzikabidhi katika Baraza la Seneti ndani ya Bunge la Marekani, Washington.

3
Kiongozi mwendesha mashtaka wa Kamati ya Usalama Mwenyekiti Adam Schiff wa Chama cha Demokrat akiongea katika ufunguzi wa mjadala katika kesi ya kumuondoa madarakani Rais Donald Trump inasikilizwa katika Baraza la Seneti.

4
Afisa muungozaji kesi Jaji Mkuu John Roberts akiwaapisha wajumbe wa Baraza la Seneti kuendesha mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump ndani ya Bunge la Marekani, mjini Washington, Alhamisi, Jan. 16, 2020. (Senate Television via AP)