Rais mpya wa Ken ya Uhuru Kenyatta has ameapishwa mbele ya umati mkubwa wa watu walomshangiria na kupeperusha bendera ya Kenya, mjini Nairobi.
Uhuru Kenyatta akabidhiwa madaraka Kenya

1
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akila kiapu huku mkewe Margaret akishikilia Biblia wakati wa sherehe rasmi kwenye uwanja wa michezo wa Kasarani Nairobi, Aprili 9, 2013.

2
Wachezaji ngoma za kitamaduni wakiwatuumbuiza wageni wakati wa sherehe rasmi za kuapishwa Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Kasarani Stadium, Nairobi, Aprili 9, 2013.

3
Rais wa Kenya anaeondoka madarakani Mwai Kibaki akikagua kwa mara ya mwisho gwaride rasmi la jeshi kabla ya kuanza ssherehe rasmi za kuapishwa rais President Uhuru Kenyatta huko uwanja wa Kasarani, Nairobi, Aprili 9, 2013.

4
Rais wa Kenya anaeondoka madarakani Mwai Kibaki akiwapungia mkono wananchi alipowasili kuhudhuria sherehe za kuapishwa Uhuru Kenyatta kwenye uwanja wa Kasarani, Nairobi, Aprili 9, 2013.