Mkuu wa kanisa la Kikatholiki, Papa Francis amewasili mjini Nairobi Jumatano jioni, Novemba 25 2015, na kupokelewa na wakuu wa serikali na wananchi, akianza ziara ya nchi tatu za Afrika. .
Papa Francis akaribishwa Nairobi

1
Wanajeshi wanashika ulinzi katika barabara ya Nairobi wakisubiri kuwasili kwa Papa Francis.

2
Wakenya walokusanyika kando ya barabara kuu kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenyatta wakisubiri kuwasili kwa Papa Francis.

3
Wafanyakazi wa Hospitali ya Mater katika njia kuu kati ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenyatta wakimsubiri Papa Francis kupita, Nov. 25, 2015.

4
Wakenya wakiwa na furaha wasubiri kumkaribisha Papa Francis.