Siku ya Jumanne, Februari 18 ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa Israel kuondoa wanajeshi wake kutoka miji iliyo kusini mwa Lebanon, kulingana na makubaliano ya kusitisha vita yaliyosimamiwa na Marekani.
Makubaliano hayo yalimaliza mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah, mwaka uliopita.
Israel imesema kwamba baadhi ya wanajeshi wake watasalia katika sehemu tano za mpaka huo, kwa maslahi ya usalama wa Israel.
Kundi la Hezbollah, ambalo lilipata pigo kubwa sana kwa kupoteza wapiganaji wake wakati wa vita, limesema Israel ilikuwa bado imekalia ardhi ya Lebanon na kwamba inaiwajibisha serikali ya Lebanon kuhakikisha wanajeshi wa Israel wanaondoka kabisa.
Forum