Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 29, 2025 Local time: 18:26

Mkuu wa jeshi la Uganda anasema nchi yake imepeleka vikosi Sudan Kusini


Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa jeshi la Uganda. (FILE PHOTO:)
Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa jeshi la Uganda. (FILE PHOTO:)

Mivutano kati ya Rais Salva Kiir na Makamu wake wa Kwanza wa Rais Riek Machar ikizusha hofu ya kurejea vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mkuu wa jeshi la Uganda amesema leo Jumanne kuwa nchi yake imepeleka vikosi maalum katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba ili kuulinda wakati mivutano kati ya Rais Salva Kiir na Makamu wake wa Kwanza wa Rais Riek Machar ikizusha hofu ya kurejea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hali ya wasiwasi imeongezeka katika siku za hivi karibuni nchini Sudan Kusini, mzalishaji mafuta baada ya serikali ya Kiir kuwatia ndani mawaziri wawili, na maafisa kadhaa waandamizi wa jeshi wanaoshirikiana na Machar.

Waziri mmoja hata hivyo ameachiliwa. Ukamataji wa Juba na mapambano yanayosababisha vifo katika mji wa kaskazini wa Nasir unaonekana kudumaza makubaliano ya amani ya mwaka 2018 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano, kati ya vikosi tiifu kwa Kiir na Machar ambavyo vimesababisha watu 400,000 kupoteza maisha.

Katika siku mbili zilizopita, vikosi vyetu maalum viliingia Juba ili kuulinda mji, mkuu wa jeshi la Uganda, Muhoozi Kainerugaba alisema katika mfululizo wa ujumbe kwenye mtandao wa X usiku wa kuamkia Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG