Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 30, 2025 Local time: 01:25

Papa anaendelea vizuri Vatican yasema


Papa Francis yuko katika hali ya utulivu anapopambana na niumonia hospitalini kwa siku ya 17 sasa, na anapumzika baada ya kuwa na usiku wa amani, Vatican imesema Jumapili.

Vatican Jumamosi jioni ilisema kwamba hali ya papa huyo mwenye umri wa miaka 88 ilitulia, baada ya kupata shida ya kupumua siku moja kabla.

“Usiku ulikuwa wa amani, Papa bado anapumzika,” ilisema barua ya mstari mmoja kutoka Vatican Jumapili asubuhi ambayo haikutoa maelezo zaidi.

Taarifa kamili ya matibabu na kuhusu hali ya Papa ilitarajiwa kutolewa Jumapili jioni kwa saa za huko.

Papa Francis alilazwa katika hospitali ya Gemelli ya Rome, Februari 14 akiwa na matatizo makubwa ya kupumua ambayo yalipungua haraka na kuwa nyumonia mara mbili, maambukizi makubwa katika mapafu yote ambayo yanaweza kuyaathiri na kuyatia makovu, na kufanya iwe vigumu kupumua.

Forum

XS
SM
MD
LG