Aliyasema hayo Rais wa Marekani Donald Trump alipokuwa akihutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Marekani kwenye jengo la Capitol Jumanne usiku.
Trump alisema “Tumefaulu zaidi katika siku 43 kuliko tawala nyingi kumiza yale yaliochukua miaka minne au miaka 8 kwa wengine – na tunaanza tu.”
Aliendelea kusema kuwa katika muda wa wiki 6 zilizopita, ametia Saini karibu Amri za Kiutendaji 200 na kuchukua hatua zaidi ya 400 ili kurejesha usalama, matumaini na utajiri kote katika nchi hii yetu nzuri.
Trump alisema kuwa “Wananchi walinichagua kufanya kazi hiyo, na ninaifanya. Kwa hakika, imeelezwa na wengi kuwa mwezi wa kwanza wa urais ndiyo wenye mafanikio makubwa katika historia ya taifa letu.”
Alisema miongoni mwa vipaumbele vyake ni kuokoa uchumi wa taifa na kupata unafuu wa haraka kwa familia zinazofanya kazi, akiongezea kuwa wamerithi kutoka kwa utawala uliopita, janga la uchumi, na jinamizi la mfumuko wa bei. Alidai kuwa sera za waliotangulia zilipandisha bei ya nishati, ziliongeza gharama ya mboga, na kufanya mahitaji ya maisha yasiweze kufikiwa na mamilioni ya Wamarekani.
Aliongezea kusema kuwa kama Rais, anapambana kila siku kubadilisha uharibifu uliofanyika na kuifanya Marekani iwe na nafuu tena.
Alizungumzia bei ya mayai akisema kuwa Joe Biden aliruhusu bei ya mayai isidhibitiwe – na hivi sasa utawala wake unajitahidi kushusha bei hiyo. Akisema kuwa lengo lake kuu la mapambano hayo ni kushinda mfumuko wa bei na kupunguza gharama ya nishati.
|
Forum