Afrika Kusini inasema kwamba Marekani inajiondoa katika mpango wa kufadhili athari za mabadiliko ya hali ya hewa uliofikiwa na mataifa tajiri kuzisaidia nchi zinazoendelea kuachana na matumizi ya mkaa na kuanza kutumia nishati mbadala.
Rais Donald Trump akiwa amesaini amri ya utendaji.
Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini inaeleza kwamba imepokea uamuzi wa marekani kujiondoa kutoka mpango huo wa JETP, kufuatia amri ya utendaji iliyotiwa saini na Rais Donald Trump.
Afrika Kusini ambayo inategemea zaidi mkaa kwa ajili ya kuzalisha umeme ilijiunga na JETP 2021 kwa lengo la kupata msaada wa kupunguza matumizi ya mkaa na kugeukia matumizi ya nishati safi mbadala.
Marekani iliahidi kutoa dola milioni 56 kwa mpango huo na kuongeza dola bilioni 1 kwa ajili ya uwekezaji wa kibiashara.
Nchi nyengine zinazopokea msaada kutokana na mpango huo ni Senegal, Vietnam na Indonesia.